Shirika la Rafiki-SDO kupitia mradi wa KUTOKOMEZA AJIRA ZA UTOTONI MAENEO YA MIGODINI limetoa mafunzo kwa wajasiliamali ( new comers and YBC trainers) waliopo kituo cha vijana cha Biashara Nyangalata kwa kushirikiana na YEP Tanzania
Read moreVijana kutoka kituo cha biashara cha Nyangalata wamepatiwa mafunzo hayo kupitia mradi wa KUTOKOMEZA AJIRA ZA UTOTONI MAENEO YA MIGODINI ikiwemo ushonaji.Mradi huo unatekelezwa na shirika la RAFIKI SDO kuwawezesha vijana kiuchumi na kutimiza ndoto zao.
Read moreWafanyakazi wa Shirika la RAFIKI SDO wakiwa Butiama kuelekea Musoma kuhudhuria kikao kazi cha kila mwaka ambacho huwakutanisha wafanyakazi wote kujadili shughuli za miradi mbalimbali zinazotekelezwa na shirika kwa ujumla wake kwa kipindi cha mwaka mzima.Siku hii hufahamika kama siku ya familia ya RAFIKI SDO.
Read moreMkurugenzi Mtendaji Gerald Ng`ong`a wa kwanza kutoka kushoto akipata maelezo kutoka kwa afisa takwimu(katikati) na kulia ni Afisa Tabibu juu ya zoezi la uhakiki wa takwimu wakati alipofanya ziara ya kushitukiza kujionea utendaji kazi katika zahanati ya Kizumbi mahali shirika la RAFIKI SDO linatekeleza afua ya kitabibu ngazi ya jamii kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Shinyanga.
Read moreShirika la RAFIKI SDO linalotekeleza mradi wa TUWALEE wilaya ya Shinyanga, Kutokomeza mila kandamizi dhidi ya mtoto wa kike katika kata ya Ilola limetoa Elimu hiyo kupitia makundi mbalimbali na kujadiliana namna bora ya kuachana na mila zinazo mkandamiza mtoto wa kike na kuzuia ndoa na mimba za utotoni katika jamii.
Read moreShirika la RAFIKI SDO limetoa baiskeli kwa wawezeshaji wa vikundi vya mabinti afua ya kiuchumi ngazi ya jamii ili kuhakikisha wanawafikia mabinti hao kwa wakati. Zoezi la ugawaji wa baiskeli lilifanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.Wawezeshaji hao kutoka wilaya ya Shinyanga na manispaa ya Shinyanga walisema kuwa vifaa hivi vitarahisisha kuwafikia walengwa katika kata zao kwa wakati.
Read more